Friday 30 September 2016

Hizi ndio smartphone zenye gharama kubwa duniani 2016

10.vertu signature Diamond($88300) 

Simu hii gharama yake haitegemei na vitu(features) zilizopo bali kwani ina features chache lakini muundo wake na rangi ya simu huu ndio huifanya iwe simu ghali duniani kwani imenakishiwa na(diamond colour)

9.IPhone Princess plus($176,400)

Simu hii imetengenezwa na kampuni kubwa duniani ya apple,simu zote za kampuni hii zinamfumo(operating system) tofauti na mifumo ya simu nyingi.Simu hii inamuonekano mzuri na wenye kuvutia na ndio maana wakaamua kuiita “princess”.Bwana Peter Alvison ndio aliyeunda(design) simu hii ghali duniani

8.Black Diamond VIPN smartphone(3000,000)

Simu hii imetengenezwa na kampuni ya Sony Ericsson,simu hii imetengenezwa kwa ustadi mkubwa sana kwani ina muundo(features) nyingi sana ikiwemo polycarbonate mirrors na Organic Light Emitting Diode (LED) .Kioo cha simu hii ni imara sana na kuwa simu yenye kioo kigumu kuliko smartphone zingine duniani,uwepo wa diamond kwenye navigation button na nyingine nyuma ya simu ndio huifanya simu hii kuwa na gharama ya juu.

7.Vertu Signature Cobra($310,000)

Jina la simu hii ni kutokana na muundo wake wa nje kwani imenakishiwa kwa umahiri mkubwa sana(muonekano wa cobra sehemu ya mbele ya simu).simu hii imetengenezwa na madini aina ya rubi(four hundred and nine pure rubies).

6.Gresso Luxor Las Vegas jackpot(($ 1 million)

Simu hii imetengeneza na(bleach diamond na bleach African wood).Kwa wale wapenda smartphone zenye sifa nzingi(specifications) basi simu hii pamoja ni ya gharama ya juu simu haina sifa nyingi sana 

5.Diamond Crypto smartphone($1.3 million) 

Simu hii ni simu yenye hadhi sana hasa kwenye maeneo yenye mkusanyiko mkubwa mfano kwenye sherehe,matamasha hii ni kutokana na kuwa na muonekano mzuri machoni mwa watu.Simu hii imetengenezwa na (pure and solid platinum),ikiwa na 18 carat gold navigation key ambapo vipande 28 vya diamond vimetumika pembeni ya simu hii ili kuifanya iwe na muonekanao wa kuvutia,pia uwepo wa princess diamond hufanya iwe simu yenye gharama kubwa.

4.Goldvish Le million($ 1.3 million)

Bwana Emanuel Gueit ndio mtengenezaji wa hii simu,simu hii imetengenezwa kwa dhahabu halisi(white pure gold).Simu hii ni miongoni mwa simu zinazotengenezwa kwa oda maalumu

3.Iphone 3G King Button($ 1.5)

Simu hii ina(high quality 6.6 carat diamonds,yellow gold na rose gold) ivyo vyote kwa pamoja hufanya simu hii kuwa na muonekano wa kuvutia


2.IPhone 5 Black Diamond($15.3million)

Hii ni simu ya pili kwa gharama duniani,ukumbukwe kwamba upatikanaji wa black diamond ni mgumu sana duniani ndio maana simu hii gharama yake ni ya juu sana kutakana na kutengenezwa kwa na black diamond.


1.Falcon  Super Nova Pink Diamond IPhone 6 ($95.5million)

Uwepo wa (18carat of huge diamond) ndio huifanya kuwa ndio simu(smartphone) ya kwanza ghali duniani,simu hii pia imetengenezwa na kampuni ya apple kwa ustadi mkubwa sana na inatengenezwa kwa oda maalumu(special order)

Wednesday 28 September 2016

Ally kiba kuwania tuzo MTV EMA 2016

Hatimaye msanii wa miondoko ya bongo flavor alimaarufu kama Ally kiba anayetamba na kibao chake cha "Aje" atajwa kuwania tuzo izo kubwa katika kipengere cha "Best African Act ".Ambapo tuzo iyo mwaka jana ilichukuliwa na mshindani wake mkubwa Diamond platnumz na kuweka historia ya kuwa mwafrika wa kwanza kuchukua tuzo iyo tangu zianzishwe.Katika tuzo izo Ally kiba akiwa ni mwakilishi pekee toka Tanzania kwa mwaka huu,ukilinganisha na washindani wenzake katika kipengele icho ambapo kuna wasanii wakubwa barani afrika akiwemo wizkid(Nigeria),Olamide(Nigeria),Casper na Black coffee wote kutoka Afrika kusini

"MUNGU IBARIKI AFRICA"
"MUNGU IBARIKI TANZANIA"

Tuesday 27 September 2016

Mahaba ya treysongz na vanesa mdee

Mwanamziki maarufu nchini marekani wa miondoko ya Rnb treysongz na mwanadada mrembo wa miondo ya bongo flavor anayetamba na kibao chake niroge vanessa mdee picha zao zenye utata za vuja kwenye mitandao ya kijamii wakiwa katika mazingira ya kimahaba yapo kuwa wawili hao wanadai kuna ngoma wamefanya na ivi punde itatolewa ,,,,,,,katika hali isiyo ya kawaida wasanii hao wakiwa katika picha ya pamoja kitandani ya zua utata kwenye mitandao iyo ya kijamii watu wakihoji kurikoni,,,??!! Je ni collabo ama kuna kingine zaidi ya collabo..??!! Daima wazungu wanasema "time will tell you"

Maneno ya davido baada ya jina lake kutokutajwa kuwania tuzo yoyote Mtv

Mkali uyo wa kibao cha skelewi kilichotikisa barani afrika atoa neno baada ya shabiki yake mmoja kuccoment kwenye twitter,,,,,,,,,,,baadaya muda mfupi davido aliamua kujibu "i really shouldn't be nominated this for what??.I got three MAMAs in two years i'm good still gonna be a great show!. But next years


Haya ndio maneno aliyoyasema mrisho mpoto kwa diamondplatnumz

Salome ya Diamond imezidi kupata heshima kubwa ndani na nje ya nchi na inawezekana ikawa ni tofauti na mwenyewe alivyotegemea. Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto amedai kufurahishwa na wimbo huo kutokana na kuwa na ladha ya Tanzania.

Mpoto amediriki kusema hayo kupitia mtandao wake wa Instagram wikiendi hii huku akiendelea kwa kumpongeza msanii huyo kwa kuutangaza muziki wa Bongo Fleva na kuiletea heshima Tanzania.

“Nassibu kiukweli nimefurahishwa sana na kazi yako ya #Salome imeonyesha ukomavu Mkubwa na team work, kikubwa ukiwa unafanya kazi zenye test ya nyumbani unatupa heshima kama nchi na inakuonyesha wewe ni nani? na nani siyo wewe?,” ameandika Mpoto kwenye mtandao huo.

“Nassibu Mwenda kwao siku zote haogopi Giza, nenda lakini waambie nna kwetu, kama ulivyofanya kwenye Salome. Sisi ni wabantu bwana tunaruhusiwa zaidi ya mmoja, na Mimi ntamtafuta Salome wangu wa ukubwani ashike magoti nisimame kama ngongoti japo nna kitambi ntainama kidogo!!.

Wanafunzi wa fani za afya

Kwa wale wanafunzi wa fani za afya wanakaribishwa chuo bora kabisa cha Kilimanjaro Christian medical university college,chuo ni kizuri na kinapatikana mazingira mazuri